RayVanny |
Msanii kutoka label ya WCB, Rayvanny amefunguka na kueleza kuwa kiasi kikubwa alichiwahi kulipwa kutokana na kuandikia wasanii nyimbo ni Sh. milioni moja.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma‘Unaibiwa’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa licha ya kulipwa fedha hizo kazi nyingi zilikuwa halipwi.
“Nilikuwa napewa hela ya kuunga unga wakati mwingine akijisikia ananitoa vizuri lakini nilikuwa sipati hela hiyo. kiwango kikubwa nilipata ni milioni moja” amesema Rayvanny.
Ameendelea kusema kuwa kwa sasa hivi amesitisha kuandika utaratibu huo kwani anaandika ngoma zake ila akiwa studio na wasanii wenzake huwa wanasaidiana.
Comments
Post a Comment