SEHEMU YA 2
Ilipoishia,,Habiba
alikua ameaga anaenda chuo kuangalia matokeo ya walio chaguliwa kujiunga na
chuo cha kumbukumbu. Ya mwalimu nyerere, huko kigamboni habiba anafanikiwa
kufika kigamboni lakini sio kwa lengo lakwenda chuo bali kwenda kukutana na
james, baada ya muda wanaenda gest na james wanafanya mapenzi, huku habiba
akiwa bado hajalisahau penzi la kevi, wanamaliza habiba anamuaga james na
safari yakurudi nyumbani kwao mwananyamala inaanza, habiba anafanikiwa kufika
nyumbani lakini anamkuta dada yake akiwa nje kasimama na mwanaume wakiwa
wanapigana kiss, ana washtua baada ya kumuona vizuri yule mwanaume habiba
anapata mshtuko mkubwa na kudondoka, endelea nayo............" Habiba
vipi" dada yangu Batuli aliniuliza kwa mshangao maanake nilipo muona bwana
ake nilishindwa cha kufanya, nikaishia kudondoka, " hamna kitu" ndilo
jibu nililo mpa Batuli, sikufanya kitu lakini nilikimbia kuelekea nyumbani,
roho ilikua inaniuma vibaya mno yaani maafa yalikua yametawala moyoni mwangu,
yaani kweli dunia chungu lakini mbona kwangu mimi tuu, wakati nawaza yote
hayo kulikua kuna begi dogo lilikua linadawa za bibi alizokua akipewa
hospitali, nilizichukua kama zilivyo, kisha nikafunga mlango wangu vizuri
nikazibwia zile dawa, haikua tabu sana kufanikisha zoezi la kujiua, nilikaa
kama dakika mbili nikaanza kuhisi utofauti,,kufa jamani we kuskie tuu, mwili
wote ulikua umechoka sijiwezi sina hali nikawa napiga kelele za kuomba
msaada,,"nakufa nakufa nakufa" hakuna chochote kilichotokea nilienda
kuufungua mlango ili niweze kutoka kukimbia lakini wapi, nikazidiwa nikalala
pale chini yaani moyo ulikua sio wangu,,
Ghafla
nikazinduka lakini sio nyumbani ilikua hospitali,, wakati sina hili wala lile
nilimuona baba kwa mbali akiwa anaongea na maaskari, dada batuli alikua pembeni
yangu alikua anasinzia sikutaka kumuamsha nilikua nashangaa imekuaje, nilivizia
baba aje niongee nae kua hapa nimefikaje, mbona sielewi,, ghafla nikakumbuka
tukio zima,, nikahisi kama mkojo unataka kunitoka, mungu wangu nilikua nataka
kujiua, na ndio maana nimeletwa hapa hospitali yale madonge niliyomeza, sijui
itakuaje,, baba ataniua maana nimemtoa mkoani,, alikua morogora kazini nahisi
mamkubwa itakua alimpigia simu, Habiba mimi mbona mikosi inanifuata,, sikutaka
hata kumshtua tena baba maana angeni gombeza sana namjua anamaneno makali
sana,, nikajifanya nimelala huku nikiwa namchungulia kiwizi wizi,,basi
alimalizana na yule polisi kisha akaja mpaka pale kitandani nilipo lala,
alimuamsha batuli kwanza,," Batuli, Batuli Batuli" batuli aliamka
"nenda kalale dereva wa bajaji yupo nje atakupeleka nyumbani niache mimi
nitamuangalia dada yako", Batuli alikataa" baba we acha tu
nimuangalie mimi siunajua sisi wanawake naweza kumsaidia kwenda chooni, na vitu
vingine we niache mimi", Baba alipatwa na hasira kusikia vile akaanza
kumfokea batuli,," wewe umeacha mpaka mdogo wako anataka kufa sasaivi
unadai nikuache umuangalie, hapa ulipo unalala lala tuu, mwanangu angekufa
mngenieleza nyie,, mdogo wako mpaka anakunywa sumu we ulikua wapi chanzo ni
nini hujui sasa nitakuachia vipi umuangalie" Batuli alinywea kimyaa
Batuli muongeaji lakini ujanja wote ulikua mfukoni, mimi hapo naskia maneno
yoote yanayotamkwa na baba, huku roho inanidunda, nikasema nikijifanya
kuamka tuu mimi maiti maana batuli kaambiwa hivi mimi je sijui itakuaje?
Nikajikausha kimyaa mtoto wakike, batuli akaondoka zake nikasema mama yangu
kimoyo moyo bora angebaki batuli hapa leo sijui itakuaje,, ilikua mida ya saa
tatu usiku mamkubwa alikua kaja na vyakula pale hospitalini uzuri hospitali sio
mbali, ni pale pale mwananyamala hospitali,, nesi aliwaambia waniamshe nile
chakula, ,nilikua naskia kila kitu ila ikanibidi nizuge afadhali lakini mama
mkubwa alikua kesha fika manaake ingekuaje sijui mimi na huyu mzee,,"
Habiba Habiba Habiba mama" ,ulikua msauti wa mzee nilijivuta nikajivuta
tena kisha nikaaamka kwa utaratibu saana,," taratibu mama inuka ule"
, mzee alikua ananipenda sana sema basi tu mimi mwenyewe nilikua sijatulia,
hata ivyo sikuamini kama angenijali sana kiasi kile," shikamoo Baba"
nilimuamkia si unajua tena ndio naamka na sijamuona siku nzima ilinibidi nizuge
hivyo," marahaba Mama haya ebu kaa vizuri uanze kula sasa" niliamka
nikaanza kula hakuna kitu hata kimoja nilichosemeshwa juu ya tukio nilipomaliza
kula mzee alinisihi nipumzike, we acha tu nikajifanya kulala tena,,, asubuhi
nililetewa juicy kubwa ya maembe na supu ya kuku,, nikawa mpaka naona aibu hivi
kweli nastahili huduma hizi zote,, mzee wa watu babaangu alikua analala huku
kakaa na mbu wa pale mwananyamala daa kwakweli nilimuonea huruma, , baadae nesi
alikuja nakutuambia kua tumeruhusiwa chamsingi ni kuzingatia dawa na kuto mpa
mgonjwa presha au stori za kumfanya akose raha,, basi mzee alinipakiza kwenye
gari yake mpaka nyumbani nilikaa sebleni kidogo kisha nikaingia chumbani,
Huyu kevi jamani ananitakia nini mimi ameona haitoshi kuniacha mimi
kaamua kumchukua na dada yangu batuli, huyu mbwa mwanaharamu alikua anataka
kuniua, siwezi kumsamehe kamwe kwa kitendo alichonifanyia,,yule aliekua
anapigana kiss na dada yangu alikua ni kevi na ndio kisa cha mimi kuanguka na
kutaka kujiua amakweli mapenzi, yaskie tuu, mwanamke nimekosa raha amani yaani
sielewi ulimwengu unaendaje,,lakini sikutaka mtu ajue stori ile kua nilitaka
kujiua kisa kevi au kisa mapenzi, nahisi Batuli alikua anajua lakini sina
uhakika sijui kevi kamwambiaje itakua kamdanganya tuu, daa nyie wanaume kweli
sumu najuta kujiingiza kwenye mapenzi,, sikutaka kukaa sana chumbani ilinibidi
nitoke kwenda sebuleni ili wasije kusema pengine nataka kujiua tena, ile natoka
tuu namkuta james yupo sebleni na baba sijui kuna nini james hajawai kufika
kwetu na hapajui sijawai kumuelekeza sasa kafikaje na nani kamleta maswali
mengi nilikua najiuliza kichwani yaani nakosa majibu, ikabidi mzee aanze
kuongea sasa alikua yupo batuli mama mkubwa na ndugu kama wawili ivi na james
pia, " sasa bwana james mwenzako amepata matatizo kidogo sijui kama
unafahamu ila ndio ametoka hospitali muda si mrefu, sijui ni nini kilimpata
maana alikua amefikia hatua ya kukata tamaa na maisha, nimejaribu kumuuliza
mama yake mkubwa na dada yake wakasema hawafahamu kitu ndipo polisi mmoja
akatupa ushauri tuangalie simu yake mpaka anapatwa na tukio la kutaka kukatisha
maisha yake wewe ndio ulikua mtu wa mwisho kuongea nae na mesej tumeziona najua
nyinyi ni vijana lakini cha msingi naomba uniambie mmekwaruzana nini":
wakati james anajiuma uma kujibu nilidakia haraka," hamna baba mimi
kwakweli nilikua nimeenda chuo kuangalia matokeo yangu kama nimechaguliwa
nilipoona sijachaguliwa ndio nikawa ninamawazo mengi rafiki zangu walikua
wamechaguliwa kwakeli nilijiskia vibaya ndio maana nikachukua uamuzi ule wa
kijinga," niliongopa kwa staili hiyo lakini huku moyo ukiwa unaenda mbio
sana, baba ilibidi aanze kunisema " sasa mwanangu swala hilo mbona dogo
sana unataka kujiua ili iweje sasa unajua utaniua mimi sasa badala ya kujiua
wewe sasa, hilo sio tatizo kabisa cha msingi ungenitaarifu mimi ningejua
nikusaidiaje nasio uamuzi uliouchukua, siumeomba chuo cha kumbukumbu ya mwalimu
nyerere pale kigamboni" ndio baba " nilijibu upesi huku nikiwa
nanyonga nyonga vidole vyangu," mbona pale mimi najuana na watu wengi sana
wewe niachie mimi, chuo hesabu umepata lakini siku nyingine usirudie sawa"
aliishia hivyo." Sawa" nilimjibu kwa haraka, watu wote
wakaondokewa na hofu maana kwa kuwaangalia tuu walikua wanajua ni swala la
mapenzi lakini nikawa nimeubadili mchezo kiufundi na kwa haraka zaidi kwakweli
habiba mimi na huu uongo napaswa kua muigizaji,,kwa kuangalia tuu sura ya
batuli alikua hajaridhika kabisa na kisingizio nilichokitoa alikua anajua
nimeongopa lakini hakusema kitu na mimi sikumjali hata kidogo, basi mzee
aliendelea kupiga stori pale ikawa burudani, maskini james najua anavyojiskia
mkaka wa watu najua ikikua ni zaidi ya balaa kwake maswali kibao yalikua
kichwani mwake lakini ntaongea nae baadae," james, mwanangu nampenda
sana lakini nikiskia umemuudhi au kumpiga itabidi udili na mimi lakini naomba
umpende kama anavyokupenda mimi najua kila kitu ila cha msingi muwe makini na
mkazane kwenye masomo, naskia nawewe umeomba chuo cha mwalimu nyerere"
ndio" james alimjibu mzee, " vipi wewe umefanikiwa" mzee
alimuuliza tena," aah nashukuru mungu nimefanikiwa" mzee alirudisha
jibu" basi hongera ngoja na mimi nimtafutie huyu nafasi hapo mwalimu
nyerere, ila msome sio muoane huko" mzee alimaliza kisha akaendelea
nashughuli zake, sebuleni nikaachwa mimi na james tuu lakini ilikua utata
kidogo maana james alikua anataka kujua mkasa mzima na mimi nilikua staki
kumuambia kila kitu, nilimdanganya tu kuwa kulikua kuna kaugomvi baina ya mimi
na dada yangu kwaio ndio nikaamua kutaka kujiua lakini yameisha yale sasa ivi
naangalia mambo mengine, mimi kwauongo tena, yeye mwenyewe alinielewa, akaacha
kuniuliza, basi nikamsindikiza ili akapande gari zakuelekea kwao, alikua
anapanda gari za mwana nyamala kivukoni kwa kua alikua anakaa kigamboni, wakati
namsindikiza nikakutana na Kevi barabarani nilimuangalia sana kevi, james pia
aligundua kitu, aliniuliza swali kua vipi namjua yule jamaa, nilimjibu
hapana" dhaa yule jamaa nikikuadisia stori yake huwezi kuamini anastori
yakutisha kule kigamboni kaacha jina" wakati james ananiadisia hayo
linakuja gari la mwananyamala karibu yetu likiwa tupu na james anaamua kupanda
gari lile, ananiacha na maswali mengi sana nakua naumiza kichwa nasipati jibu
lakini daaah mungu wangu sasa itakuaje asije kua ni muuaji yule jamaa itakua
balaa mbona huyu kevi anasiri nzito sana kwakeli siwez kuvumilia ngoja nikifika
nyumbani nimpigie simu james nijue alitaka kuniambia nini kuhusu kevi na
anasiri gani nzito kaacha jina gani mtaani kwao? nilikua nina maswali lukuki
kichwani nilienda kununua vocha ya elfu moja nikaiweka kabisa kwenye simu, ili
nivizie mida ya kujirusha usiku na tigo niongee nae james kwa kina kuhisu stori
ya huyo kevii nilikua nina wasiwasi kama napokea majibu ya vipimo vya ukimwi,
huyu kevi itakua kafanya nini mbona sielewi, mungu si athumani saa nne ikafika
nikampigia simu james, simu yake ilikua inaita tuu wala haipokelewi, baadae
nikakata tamaa, ya kumpigia , saa nne kama na nusu ivi akapiga simu, alikua
ananiomba samahani kwa kutopokea simu mimi sikujali nilikua nataka stori ya
kevi tu basi sikuwai kumfeel james hata kidogo nilikua najua ni mcheshi
mtaratibu lakini nilikua nimekufa na nimeoza kwa kevi, " sawa dia usihofu
nimekuelewa usijali" nilimvuta vuta james ili anipe tuu uhondo, wa stori
kuhusu kevi," vipi dia ulisema unamjua yule jamaa na ulisema kafanya
vituko vipi kwani kafanya nini?" Nilidadisi kinafiki, ili nijue tuu ukweli
" yule jamaa bwana anatembea na wake za watu juzi juzi kafumwa ukawa msala
zaidi alafu inasemekana jamaa anamchezo wakuwapiga picha wanawake anaotembea
nao nakwenda kuuza magazetini hizo picha ni zautupu na huwa ana zirusha
mitandaoni" mtumeee nimekwisha nakumbuka kevi alikua ananiambia
nigeuke anipige picha na siku nyingine ananipiga picha nikiwa naoga nae na
nyingine alikua ananinyoa, mungu wangu nimekwisha, wakati nawaza hayo
niliendelea kumsikiliza james" duu kweli ni balaa huyo jamaa"
nilisema kinafki ili stori ziendelee huku nikiwa naumia kwa kua na mimi ni
muhusika pia, " Wewe unashangaa hilo mbona dogo jamaa inasemekana
anasambaza ukimwi yaani kama mpo waschana watatu au wanne nyumba moja lazima
atembee nao wote nawote awaambukize,"mwili wote ulikufa ganzi nikawa
simsikii tena james nikakata simu nikawa nimejilaza hivi, sasa nikawa nimepata
sababu nzuri yakujiua
Comments
Post a Comment