Mwishoni mwa msimu uliopita klabu ya Man United ya England ilifanikiwa kuingia mkataba wa udhamini na kampuni ya Adidas katika kutumia jezi zao, mkataba wa Man United na Adidas ni wa miaka 10 na unaripotiwa kuwa na thamani ya pound milioni 750.
Katika mkataba huo wa Man United na Adidas una kipengele kama Man Unitedwasipofanikiwa kumaliza katika top 4 EPL na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa pili Adidas watapunguza asilimia 30 ya mapato yao ya mwaka ambazo ni zaidi ya pound milioni 20 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 54.
Kwa sasa Man United wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 tofauti ya point sita na aliyepo nafasi ya nne, afisa wa masuala ya fedha wa Man United Cliff Baty ndio alithibitisha taarifa za uwepo wa kipengele hicho.
Comments
Post a Comment