Ndege mpya iliyonunuliwa na Serikali ya Rwanda kutoka Marekani

Shirika la ndege la Rwanda linazidi kuchukua nafasi ya kujiimarisha kwa safari za kimataifa na sasa limenunua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next Gen. Ndege hiyo imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali nchi Rwanda Jumatano usiku ikitokea Marekani.
Ndege hiyo inakua ni ya pili mfululizo kununuliwa na serikali ya Rwanda chini ya Rais Kagame ambaye alitangaza kulifanyia mabadiliko makubwa shirika la ndege la nchi hiyo RwandAir kwa lengo la kuongeza mapato ya usafiri wa anga.
Ndege hii imetajwa kuwa na sifa za kutumia mafuta kiasi kidogo huku iruhusu abiria kutumia wireless internet ya Wi-Fi wakiwa ndani ya ndege hiyo. Rwanda inakua ni nchi ya kwanza barani Afrika kumiliki ndege ya aina hiyo na nchi ya pili duniani baada ya Marekani.
Nimekuwekea hapa Video ya mapokezi ya ndege hiyo nchini Rwanda.

Comments