Steven Gerrard agoma kusaini mkataba mpya na LA Galaxy



Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ametangaza kuwa hata saini mkataba mpya na timu yake ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya Marekani.
Gerrard (36) alijiunga na Galaxy mwaka 2015 na amefunga magoli matano kati ya mechi 34 alizocheza katika misimu yake miwili akiwa na timu yake hiyo huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwezi ujao.
“Kwa hakika si mwisho wa maisha yangu katika soka” amesema Gerrard. “Sasa natizamia kwenda nyumbani kutumia muda na familia yangu, nikiwa nazingatia hatua nyingine ijayo.”
Gerrard hapo awali iliripotiwa kuwa atarejea Anfield katika majukumu ya ukocha huku ripoti zingine zikisema kuwa atajiunga na kocha wake wa zamani Brendan Rodgers katika klabu ya Celtic.

Comments