Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi leo asubuhi mkoani Morogoro na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero mkoani humo.
Nay wa Mitego amekamatwa akiwa hotelini Morogoro baada ya kuamaliza shughuli zake zilizompeleka ambapo alitakiwa kuongozana na polisi hao hadi kituo cha polisi.
“Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote. ✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo.” Ameandika Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Licha ya kuwa mwanamuziki huyo hajaeleza sababu ya kukamatwa kwake, au Jeshi la Polisi kutoa taarifa, lakini inaaminika kuwa sababu kubwa ni wimbo wake alioutoa siku za hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wapo.
Wimbo huo umezungumzia mambo mengi hasa ya kisiasa yanayoendelea nchini kwa sasa ikiwa ni pamoja na tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uhuru wa vyombo vya habari na masuala ya sanaa.
Comments
Post a Comment