Askofu
wa Kanisa Katoliki Ngara, Severin Niwemugizi amesema yuko tayari kuitwa
mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za binadamu watachukuliwa
kama wachochezi.
Askofu
Niwemugiza amesema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili,
haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.
Akifungua
mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya leo
Jumatano, Askofu Niwemugizi amesema imefika wakati nchi inahitaji kuwa
na dira nzuri.
Amesema
hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye
machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.
Askofu
Niwemugizi amesema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo
katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni
ishara mbaya.
"Hizi
sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira
mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira
njema ambayo ni Katiba."
Amesema
anatambua jitihada anazofanya Rais John Magufuli katika kupambana na
ufisadi na kutaka rasilimali ziwanufaishe wanyonge lakini ni muhimu
juhudi hizo zilindwe na Katiba nzuri.
"Rais
anafanya mengi mazuri na alipoanza kila mmoja aliona dalili za
matumaini lakini juhudi hizo zinaweza zisiwe endelevu kama hakuna ulinzi
wa Katiba,”
"Tunahitaji Katiba tena Katiba nzuri ambayo haitaruhusu kuchezewa na yeyote kwa maslahi au matakwa yake binafsi."
Amesema,
"Namshauri Rais achunguze kwa makini yatakayozungumzwa kwenye mkutano
huu, ayaone kuwa yana nia njema na ayafanyie kazi."
Comments
Post a Comment