Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga R.P.C Benedict Michael Wakulyamba, amepiga
marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo
kuhamasisha uhalifu.
Akiongea
ofisini kwake R.P.C Benedict amesema miongoni mwa viashiria vya
uvunjivu wa amani ni Vigodoro, ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye
umri mdogo wakijiandaa kufanya uhalifu.
“Miziki
ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata
washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili
ya kufanya uhalifu”, amesema R.P.C Benedict.
Hata
hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya
kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda
utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili.
Comments
Post a Comment