Kampuni
ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL) inayomiliki magazeti ya
Mwanahalisi, Mawio na Mseto imesema itafungua kesi mahakamani endapo
Serikali haitaondoa zuio la kulifungia kwa miaka miwili Mwanahalisi.
Kampuni
hiyo imesema endapo leo na kesho Serikali haitalifungulia gazeti hilo
watafungua kesi na kuiomba Mahakama ifute zuio hilo na kudai fidia ya
Sh41 milioni kwa kila chapisho tangu zuio lilipoanza kutekelezwa.
Septemba
19, Serikali ilitangaza kulifungia gazeti hilo ikisema hatua hiyo
imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na
sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na
kuhatarisha usalama wa Taifa.
Mhariri
Mtendaji wa Mwanahalisi, Saed Kubenea leo Jumatano katika mkutano na
waandishi wa habari amesema gazeti hilo kwa miaka 12 tangu lianzishwe
haliandiki upotoshaji bali ukweli.
Kubenea
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo amesema kufungiwa kwa magazeti ya
kampuni hiyo ni uonevu licha ya kukiri baadhi ya maonyo waliyopewa na
Serikali.
Kubenea amesema habari zilizotumika kulifungia gazeti hilo ni za ukweli.
Comments
Post a Comment