Wakati dunia nzima ikishangazwa na majigambo kutoka kwa Marais wawili
waliojaaliwa maneno mengi yaani Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais
wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un wakitambiana kuna uwezekano mkubwa vita
hiyo inayosubiriwa na watu wengi isitokee na Marekani ikahamishia hasira
zake Iran.
Hakuna ubishi kuwa kwa sasa Marekani haina mpango wowote wa kupigana na Korea Kaskazini inachokifanya ni kuongeza vikwazo vya kiuchumi kwa taifa hilo.
Je, ni kweli Marekani inaiogopa Korea Kaskani?
Jibu ni kwamba Marekani haina kitu chochote cha kuiogopa Korea Kaskazini kuanzia uwezo wa majeshi na hata uwezo wa silaha za kivita hilo halipingiki, lakini kamwe Marekani hawezi kuja kuishambulia nchi hiyo hii yote ni kwa kuhofia usalama wa mataifa ya jirani na nchi hiyo ambao ni marafiki wakubwa wa Marekani kibiashara kama Korea Kusini na China pia vita hiyo bila shaka yoyote kutokana na silaha za nyuklia basi mataifa yote jirani ya Korea Kaskazini lazima watu wasio na hatia wataangamia.
Ilikuwa ni mwezi Agosti Rais wa Marekani, Donald Trump alipoonesha hisia zake kali kwa kumpiga mkwara Rais Kim Jong Un kuwa akijaribu tena kutoa vitisho kwa Marekani na nchi washirika wake basi jeshi lake lipo tayari kuishambulia nchi hiyo lakini wapi Rais Kim aliendelea kuongeza mkwara tena kwa kutishia kuvishambulia visiwa vya Guami vilivyopo nchini Marekani.
Kama haitoshi mwezi huo huo Korea Kaskazini ilifanya pia jaribio lingine kwa siri la silaha nzito za bomu la Hydrogen lililopelekea tetemeko la Ardhi nchini humo na nchi za jirani kama Japan na Korea Kaskazini.
SOMA ZAIDI- Jaribio la siri la nyuklia nchini Korea Kaskazini laleta tetemeko la ardhi
Kama haitoshi tena wiki iliyopita kabla ya ufunguzi wa vikao vya umoja wa mataifa vilivyofanyika nchini Marekani, Rais Trump alirudia tena kauli za vitisho vya kuiangamiza Korea Kaskazini.
Baadae tena siku moja baada ya vitisho hivyo Marekani ikarusha ndege zake za kivita kwenye pwani ya Korea Kaskazini na kutangaza hadharani kitendo hicho.
SOMA ZAIDI- Marekani yarusha ndege za kivita Korea Kaskazini kuonesha ubabe
Kwa hali hiyo watu wengi wa masuala ya kidiplomasia duniani waliamini kuwa kwa vitisho hivyo Korea Kaskazini ingekaa kimya lakini wapi, siku moja baada ya mfululizo wa vitisho hivyo, Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Bwana Ri Yong-ho kwenye hotuba yake kwenye mkutano wa umoja wa mataifa, alitamka wazi kuwa vitendo hivyo ni vya kichokozi na kama Marekani itarudia basi ndege zake zitatunguliwa.
Hakuishia hapo pia alikiri wazi kuwa Marekani imetangaza vita na Korea Kaskazini, kauli ambayo haikuchukua hata masaa manne tayari Marekani ikatoa tamko kwa kukanusha kuwa haijatangaza vita na nchi hiyo.
SOMA ZAIDI-Marekani yakanusha kutangaza vita dhidi ya Korea Kaskazini
Ukiachana na matukio hayo Rais Trump amekuwa mara kwa mara akitweet kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa anafanya mawasiliano na Rais wa China pamoja na wa Korea Kusini kujadili jinsi ya kukabiliana na Korea Kaskazini katika kukomesha silaha za nyuklia.
Kwanini kuna uwezekano mkubwa kwa Marekani kumalizia hasira zake Iran?
Unaweza kusema Iran imejitia kimbelembele katika kuonesha makucha yake hadharani kwa kurusha makombora yake katika muda mbaya ambapo Marekani ipo kwenye mgongano mkubwa na mawazo juu ya Korea Kaskazini.
Marekani imekuwa ikiichunguza sana Iran katika mipango yake ya kutengeza silaha za nyuklia na imekuwa ikionywa mara kwa mara kuhusu hilo lakini bado imekuwa na usiri mkubwa katika mikakati ya uzalishaji wa silaha hizo haramu.
SOMA ZAIDI- Mkurugenzi wa CIA amshauri Donald Trump kuhusu mpango wa Nyuklia kwa Iran
Leo Iran anakuja kuonesha makucha yake ya silaha hizo hadharani tena katika kipindi kibaya kama hichi kwa kurusha makombora ya masafa marefu ile hali imekuwa ikionywa kila mwaka na Marekani.
Na sababu nyingine ya pili itakayoifanya Iran kushambuliwa haraka zaidi na Marekani ni chokochoko zake za kurusha makombora yanayoilenga Israel nchi ambayo kamwe Marekani haiwezi kuacha ikiandamwa bila kuingilia kati kwa hali yoyote.
Undugu uliopo kati ya Marekani na Israel kamwe hautaweza kuvurugwa na nchi yoyote ile hata kwa gharama yoyote Marekani itailinda Israel.
Sababu ya tatu ni jeografia ya Iran, ukiangalia nchi zinazoizunguuka nchi hiyo hazina urafiki wowote na Marekani na ndiyo maana hata kipindi kile cha awamu ya Rais George Bush aliweza kuingiza majeshi nchini Iraq na kurusha ndege za kivita kiurahisi hakujali kabisa kuua watu wasio na hatia.
Kwa hiyo ukiangalia kwa kina Marekani haiwezi kuitisha kwa lolote Korea Kaskazini itaishia kuchimba mkwara na kuiwekea vikwazo ila hasira zake itamalizia nchini Iran tena haraka sana pengine hata kabla ya Trump kumaliza muhula wa kwanza, endapo Iran itaendelea kufuata mkumbo wa kujaribu silaha nzito za nyuklia kama Korea Kaskazini huku ikiilenga Israel.

Comments
Post a Comment