Hamisa Mobeto |
Mwanamitindo, Hamisa Mobetto amepata shavu kwa kutajwa katika msimu wa nne wa tuzo za Starqt Awards zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine.
Hamisa ametajwa katika tuzo hizo kwa kuwania vipengele viwili ambavyo ni ‘People Choice Awards’ na ‘Super Mum’.
Tukio la ugawaji tuzo hizo linatarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka huu siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Bedford View City Hall, mjini Johannesburg nchini South Afrika.
Comments
Post a Comment