MAPITO NA RAHA ZA DUNIA SEHEMU {1}


SEHEMU YA 1
"Maisha huwa magumu pale unapopenda usipo pendwa,lakini huwa magumu zaid pale unapo kataa kukubali kua hupendwi, daa. Habiba miye sikuwahi kudhania ningekuja kugombania penzi, tena kwa mtu ambaye hanijali siwezi kuzificha hisia zangu lakini,sitaki kujidhalilisha pia,

huyu mwanaume mshenzi kani kana mbele ya umati anadai hanitaki, yeye na malaya wake walipanga kuniumiza roho yangu najuta kwa nini niliuliza swali lile la kumwambia achague kati yangu na yule malaya anampenda nani?, Ningejua ningeondoka bila kuuliza na mimi kiherehere changu na kukosa maarifa na kutokuuona ukweli ndiko kumenifanya nibwatuke,, daaah. Amakweli mtoto akililia wembe mpe na ndicho nilichokipata, leo hii kevi wakunikataa mimi kwa kunidhalilisha tena mbele za watu na mbele ya yule malaya wake amakweli nimeyaona,sinto rudia tena upumbavu ule tena kwa staili ile nimekoma nasema nimekoma"....
..."mawazo yalikua mengi sana
mpaka nilikua nashindwa kuelewa nipo wapi?, ghafla niliskia "Habiba Habiba Habiba,"
....... "nilishtuka kama mtu aliepigwa shoti ya umeme alikua ni dada yangu alikua ananishtua niliitikia kana kwamba nilikua usingizini "abeeee" kisha nikafuta machozi " ........dada...."kunamjomba wako hapa anakupa pole" ........" dada alikua ananipa taarifa zile nilikua nipo mbali sana kimawazo na wengi pale msibani walikua wananionea huruma jinsI nilivyokua nalia kwa maana nilikua nalia kupitiliza kumbe nilikua nalia kwa mambo yangu mengine tofauti na msiba japo nilikua msibani na msiba ulikua unanihusu,
......mjomba..... " pole sana habiba"......habiba....."akhasante nashukuru"..........."nilijikaza lakini nikiwa nimekaukwa na sauti kwa ajili ya kulia nilipotoa asante nilifuta tena chozi sasa sijui lilikua chozi la kumlilia bibi alie nitoka au kevi alie niacha, ilikua haieleweki, naomba bibi anisamehe sana, huko ulipo, maanaake ilikua kama laana msiba mzima nilikua namuwaza kevi kana kwamba yeye ndio alikua kafariki, baada ya masaa kadhaa tulielekea makaburini makaburi ya mwananyamala kisiwani , siunajua tena waislamu tuliikamilisha safari ya bibi kwa kumlaza kwenye nyumba yake ya milele, ilikua inauma sana kwa kweli alikua ni mtu wangu wakaribu sana nilimzoea na siri zangu nyingi alikua anazijua na kilichoniuma zaidi alikua
anamjua mpaka kevi nikikumbuka hapo machoz yananitoka zaidi. Daah!! huyu kevi kanipa donda ambalo sito weza kulisahau maishani mwangu, asubuhi sana nilijihimu nakuanza kufanya usafi wageni walikua wengi sana jana hivyo palikua pachafu sana nilifagia kudeki na kuandaa chai, baadae kama mida ya saa nne niliingia bafuni kuoga kisha nikajiandaa kidogo nikavaa baibui langu baadae, nikamfuata mama mkubwa nilikua nimeenda kuongea nae
kuhisu mambo ya chuo, nilimuomba ruksa, kuwa nataka niende chuo kuangalia majibu kama yametoka maana na mimi niliomba chuo cha kigamboni na wamesema majibu yatatoka leo kwaio nataka nikaangalie kama nimepita au lah, mama kubwa alikua si mfuatiliaji sana alinipa elfu kumi na kunisihi nisichelewe kurudi, nilimkubalia, alikua anajua kuwa nimeomba chuo cha kigamboni kile kilichopo n'gambo cha mwalimu nyerere,na nikweli ndicho.chuo nilichoomba, nilikua naishi mwananyamala kwaio nilichukua gari za mwananyamala kivukoni, nilikua nakaa kwa kopa, basi baada kama ya lisaa nikafika feri pantoni lilikua linashusha sikukaa sana feri Geti likafunguliwa tukaanza kuingia kwenye pantoni, baada kama ya dakika ishirini tukawa tunashuka kwenye pantoni, nilimuona james alikua yupo getini lakini geti la kutokea nilimfuata,naba adae tukawa tunaongozana nilienda nae umbali mrefu nikiwa kimya, sana alijaribu kunidadisi lakini hakupata jibu, nilimuongelesha mara moja tuu pale nilipomuambia nataka niende uwani mara moja, kwakweli sisi wanawake tunatabu sana, nilikua nimevaa baibui lakini nilipotoka uwani kwenye baa flani nilikua mtu mwingine nilikua nimevaa kimini cha ajabu sana,nilikua spendi kutoka vile nyumbani maana mama mkubwa angeibua maswali na lawama, james hakuongea kitu ila alikua anameza mate tuu, nilijua kwa sababu alikua
ananiangalia kwa jicho la tamaa sana, 
.....james...."umependeza"......."nilitabasamu sikumjibu kitu chochote, moja kwa moja mpaka kwenye gest ya entembe ilikua mitaa ya kwa dani karibu kidogo na kwa urasa james alikua keshalipia teyari alochofanya nikuchukua chips na mayai alivyo agiza na baadae tukaingia ndani chumba namba 9 haikua kazi sana nilisalula kila kitu nikabaki na chupi tu baada ya muda alikuja muhudumu wa gest alileta shuka na sabuni, james alivichukua kisha akafunga mlango, niliamua niwe wakwanza kuoga,nilienda kuoga na baadae kidogo jamesalinifuata, ikabidi tuoge wote ilikua ni mara yangu ya kwanza kufanya vitu vile na james nilikua nimezoea kuoga na kevi lakini hivi sasa hayupo tena nilimkumbuka kiasi flani maana yeye ndio alikua mwanaume wakwanza kufanya nae mapenzi lakini baada ya kuleta hitilafu mambo yakabadilika, ilikua ngumu kidogo kumsahau kevi lakini ilinibidi, james alikua teyari yupo hewani yaani alikua anamidadi ile mbaya, alikua ananitaka kwa kipindi kirefu lakini hakuweza kupata kitu, sababu moyo wangu na roho yangu Vyote vilikua kwa kevi, 
haikuchukua muda niliingia na james kitandani teyari kwa ajili ya pambano ilikua mechi nzito sana,lakini sikuwa na hisia hata kidogo nilikua namuwaza kevi tu, sura ya james nikaitoa kabisa lakini sikukatisha tendo sikutaka james ajue kitu, baadae kama masaa matano nilijiandaa kwa ajili ya kuondoka ilikua inabidi niwahi nyumbani, baada kama ya nusu saa nilifika nyumbani mida kama ya saa kumi nambili jioni, wakati nakaribia maeneo ya nyumbani kuna kitu kilinishangaza kidogo, nilimkuta dada yangu ananyonyana ndimi na bwana Wake, nilitaka kuwapita lakini ilinibidi nisimame kidogo kisha nigune kama kuwashtua sikuwai kumuona jamaa wake pale nyumbani lakini alikua ananiambiaga kua anaishi mitaa ya mwanyamala hospitali, nilipo guna walishtuka na kuachiana wakawa wananiangalia niliogopa na nilidondoka chini sikuamini nilichokiona".... Itaendeleaaa.......

Habiba kaona nini?
USIKOSE SEHEMU YA PILI 

Usisahau ku-follow kwa update

 

Comments