SEHEMU {3}
Ilipoishia toleo lilopita, habiba anamdadisi james kuhusu kevi, baada ya james kumwambia kua anamfahamu kevi na kwamba kevi anasifa mbaya, habiba anatamani kujua sifa za kevi lakini, ghafla gari inatokea james anapanda na kumuacha habiba akiwa na maswali mengi kichwani, habiba anampigia simu james ili kumdadisi tena hatimaye james anam
wambia habiba siri nzito inayomkatisha tamaa ya maisha, habiba anagundua kua kevi ni mchafuzi wa wanawake na anaweza akatembea na wanawake wote nyumba moja ili mradi tuu ausambaze ukimwi na awapige picha za utupu kwa maslahi yake binafsi, habiba anakata simu kisha anajilaza kitandani akiwa hana lakufanya, songa nayooo......." Habiba, habiba ,habiba"... niliskia sauti ya dada yangu aliyekua akinishtua sikujali sana lakini aliniambia niamke chai teyari..." kwani saa ngapi saizi"...niliuliza ili niwe na uhakika zaidi.." saa tatu asubuhi"... batuli hakunielewa alihisi kama sipo sawa alinitwanga swali.. " vipi kwanii?"....nilijibu kwa hofu kidogo.."hamna nilikua naota ndoto mbaya sana"..." inahusu nini hiyo ndoto"...batuli aliuliza kwa haraka huku akiwa ananidadisi kwa makini sana.."aaah nilikua naota nakimbizwa na watu hata siwajui"...."acha mawazo yako amka ukanywe chai".. nilimtoka kwa stahili ile maanake ningemwambia ukweli ingekua balaa, kusema ukweli nilikua nashindwa kutofautisha ni ndoto ama kweli maskini mimi Habiba naenda kuchanganyikiwa sasa, nilichofahamu mimi ni kwamba nina ukimwi na picha zangu sijui nani ameziona mpaka sasa yote hayo kwa ajili ya kevi, ndiooo! sikua na uhakika kama nilikua naota au lah, hivyo ilibidi niende kwenye simu yangu maana nakumbuka niliongea nasimu jana, nilipoiangalia simu yangu nilikuta missd call kama kumi. Hivi zilikua za james na mesej kama mbili, hivi, zote zilikua za james,, " mungu wangu kumbe kweli nilikua naongea na james"..njlijikuta nikijisemea kimoyo moyo sikua na jinsi, ikabidi nianze kuamini kua si ndoto tena bali ni kweli, nilifungua zile mesej kuona zilikua zinasemaje,,meseji ya kwanza ilikua inasema kama ifuatavyo..." vip mbona hupokei simu?" Meseji ya pili ndio ilionichanganya kabisa nakunifanya nianze kulia..." daaa yule jamaa inasemekana akikuacha ujue anauhakika kua kakuambukiza na picha kaziweka teyari mitandaoni kuna gazeti la ijumaa la jana naskia kunapicha kibao za hao madem ambao kevi kawapiga picha na kawaweka wakiwa uchi. Jamaa wangu analo kasema, nitakuletea kama unahitaji kuhakiki ninayo sema"...kwakweli ukisikia kufa ndio huku, sikua na hamu ya chai wala kitafunwa cha kwanza kabla sijajiua niliandika meseji kwenda kwa james....akhasante mpenzi haina haja achana nalo tuu"....nilimjibu ili asilione lile gazeti ingekua aibu kama angeiona picha yangu kwenye lile gazeti sikutaka yawe makubwa sana"..nilichofanya ni kujitanda baibui na kutoka nje bila kumsemesha mtu nilienda mpaka kwa muuza magazeti. Sehemu wanayouzia sio mbali na nyumbani hivyo nilienda haraka,,jamani nyie acheni nilikua najikaza tuu maanake nilikua mzima usoni ila nilikua maiti moyoni,..." mambooo"...nilimsalimia yule muuza magazeti sikujali salamu yake au anirudishie salamu..." gazeti la ijumaa la jana lipoo"?...yule kaka alinichomolea gazeti hilo alilokuwa kaliweka. Chini yamifuko yake mikubwa ya kubebea magazeti,,nilimpa elfu moja kisha nikaondoka zangu bila kujali chenji,,upesi upesi mpaka chumbani kwenda kuangalia ni nini kimo ndani,, juu kabisa ukurasa wa mbele palikua pameandikwa, kwa herufi kubwa..."UFUSKA WAENEA TZ"...hapo nikatekwa na kichwa cha habari nilipo endelea kusoma zaidi nikaiona picha ya Kevi pembeni yake kukiwa na habari inayosema..." Tazama mabinti 60 walio pigwa picha za utupu na bwanawao mmoja"...ile habari ilikua ukurasa wa pili,, sikuchelewa moja kwa moja mpaka ukurasa wapili,, kwakweli zile picha zinatisha. Nyie kevi ni mnyama muuaji kabisa,,basi nikaanza kuperuzi picha moja moja,, ndipo nilipo toa macho na kushangaa kukuta picha ya mwanamke flani ambaye nilimkuta na kevi na kumuambia kevi achague kati ya yule mwanamke au mimi,, picha ilikua ni ya utupu na aibu yule mdada alikua uchi japo kwenye gazeti walikua wameziba waliweka doti jeusi ili mtu asione sehenu za siri,," mungu wangu"... nikijikuta nikijisemea mwenyewe, nikaendelea kuperuzi nikaikuta picha ya mwalimu wangu wasekondari,,nikawa nashangaa tuu, baadae nikaikuta picha yangu,, nguvu zote ziliniiisha,,"daaah amakweli kevi kaniweza",, nilijisemea moyoni, ilikua ni picha ninayoikumbuka tena ilikua ni siku ambayo bibi alipelekwa muhimbili kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa kisukari,,nakumbuka nilidanganya naenda kwa shangazi, kumbe wapi nikapitia mojamoja mpaka sinza kumekucha kwenye gesti alio nielekeza kevi kua tukutane, nililia kwa uchungu kisha nikanyamaza,,bahati nzuri ile picha ilikua hainionyeshi sura kwa sana nilikua kama nakataa kupigwa ile picha nikajiziba uso kidogo hivyo haikuweza kunitoa uso mzima,, ila kwa mtu wakaribu akiangalia kwamakini ni lazma anijue kwakua ilikua imetoka vile sio mbaya nikashukuru pia,, tatizo ni jee vipi akiamua kuzitoa na nyingine itakuaje?, basi sikua najinsi ilibidi nilifiche lile gazet, asijue mtu yeyote juu ya yale mambo,,wakati natafakari hayo nikakumbuka suala la ukimwi swala ambalo lilinifanya nitafute glass moja ya maji na sumu kidogo ilikua sumu ya panya,,nilimimina kisha nikaiweka kando kidogo,,nikatoka nje kwenda kumuaga baba nilikua nataka kujiua kwa staili ya aina yake nilimuaga baba kama natoka ivi na nikamuaga mama mkubwa na batuli pia,nilitaka wajue nawapenda hata nikifa wajue nilikua nawapenda,nilikua nimeiandaa nakaratasi yangu yakujiua yaani kama nimeacha waraka flani hivi,,chakushangaza na chakutisha nilipoingia chumbani nilikuta mtoto. Mdogo wa anti yangu ana umri wa miaka kama mitano akiwa analia kwa uchungu na ile glass yangu ya sumu nikawa siioni tena pale nilipo iweka,,nilipiga kelele za ajabu sana,, nikawa nalia sana,, huku nikisema nimeua nimeua,, nimeua,, yaani mawazo yangu na fikra zangu zikawa zimehama kabisa kwangu nikawa nalalamika juu ya uamuzi nilioufanya wakuweka sumu kwenye glasi na kuiacha,, ile sumu ilikua inakama weupe flani wamaziwa nilipoichanganya na maji kidooogo,, nilijua fika Deusi, atakua kainywa ile sumu kwa sababu Deusi anatabia ya kupenda sana kula au kunywa vitu vilivyoachwa na watu na nikizingatia ule weupe alijua ni maziwa ,,sikua na jinsi nilibaki nalia mpaka hapo nilipopoteza fahamu kwa kujua nimeua mtoto washangazi,,baada ya muda nilizinduka nikiwa kitandani nilikua sijielewi kidogo, nilipoamua kwenda nje kutoka kuuliza juu ya mimi kudondoka nikakumbuka juu ya mtoto wa shangazi tumbo likaanza kuniuma, nilienda jikoni nikamkuta mamkubwa anaosha vyombo kwakweli niliogopa sana nikauliza kwa kudadisi...."mamkubwa eti umemuona Deo"...mamkubwa hakunijibu nilitaka nishtuke ila ndani ya sekunde alipaza sauti..."Deoooo. Njoo unaitwa na Dada yako".....Duuu huwezi j
Amini jinsi nilivyofarijika kuskia vile maana nilichokua nahisi ni kikubwa sana nilikua nahisi Deo amefariki kwa ile sumu nilioiweka kwenye glass...baada ya dakika moja deo alikua amefika..." Naaam"..deo aliitika ili apewe tena maelekezo kua kaitiwa nini..."dada yako anataka aongee na wewe"...mamkubwa alisistiza, basi nilimchukua Deo nikaenda nae mpaka chumbani kwangu nikawa na mdadisi kama alikua amekunywa ile glass ya maziwa lakini niligundua kua hakunywa kwasababu kwa spidi ya ile sumu asingeweza kupona ingekua kwa heri,, nilimpa shilingi miatano akanunue pipi kama kuzuga tu ili nimtoe mchezoni,alipoondoka likaja wazo kichwani mwangu lililokua linaniambia kua nisisahau kua ninaukimwi,,niliogopa sana nililiendea lile gazeti nikakuta halipo ile sehemu nilipo liweka nikasaka sana mule ndani bila mafanikio lakini wapi!! nilipotoka kwenda kumuuliza mamkubwa nilimkuta baba sebuleni kakaa analisoma lile gazeti nilitamani nimpokonye lakini sasa nitaanzaje na analomkononi kevi mzee anamfahamu lakini sio sana alishawai kuniona nae siku moja kwahio kama angemuona angejaji au angeniuliza,, wakati najiuliza yote hayo baba aliniita kwa ukali sana..."wewe hebu njoo hapa".."mungu wangu mtumee atakua kaiona ile picha yangu au kamuona kevi mama yangu nakufa leo"...nililia kimoyo moyo lakini nilijikaza nilimfuata ili nimsikilize anasemaje..." ivi wewe unamatatizo gani ni wanaume au uwehu wako ndio unatupa shida sisi hapa nyumbani mbona hatukuelewi juzi umekunywa sumu mara ukawa unalia, leo umezimia.,Tatizo ni nini hasa hebu tuambie"..." hamna tatizo baba" ...nilijibu kwa uwepesi lakini alijua kua tatizo lipo,," sasa basi kama hamna tatizo staki kuskia tena huo upuuzi wako na shule zipo karibu kufunguliwa na chuo ulichoomba nimeshakufanyia mpango pale mwezi wakumi utaanza hapo mwalimu nyerere kigamboni. Sawaaa"... alimalizia kwa msistizo kidogo lakini nilimuelewa,,sikumjali nilirudi upesi chumbani kwangu japo sikufanikiwa kuondoka na gazeti lakini nilishukuru kwa jinsi nilivyochomoka pale,,basi nikawa sina hili wala lile,, nikawa njia panda nikaamua,,nipange safari yakutoroka kwenda mkoani maana nilikua nataka aibu inikutie mbali sio pale nyumbani ukizingatia mazoezi ya kutaka kujiua yameshindikana, nilipanga nguo zangu vizuri nikaanza kuiwaza safari ya kutoroka nyumbani, ikua niondoke na fedha kidogo lakini niliona nichukue na pete na vitu vingine vya thamani kama vile pete za mama mdogo na vito vya thamani ili niuze mbeleni nikikwama kifedha,,basi nikawa nimepanga hivyo,,wakati nawaza yote hayo kunasimu iliingia nilipoipokea nikakuta miss call nilipo piga ikapokelewa na jamaa mmoja aliekua yupo makini na hapendi longo longo kwa jins sauti yake ilivyokua inaskika pamoja na uongeaji wake.." halow"...niliita kwenye simu,"..hallow samahani naomba kesho saatano tukutane magomeni nina habari ambayo inakuhusu sana fika bila kukosa na usije ukajutia baadae"....kisha simu ikakatwa nilipiga mimi ila kakata yeye,, niliduwaaa kidogo lakini sikukubali nikampigaia tena simu akawa hapatikani,, nilijiuliza sana ni nini tatizo au kuna ugomvi kunakitu cha kubadilisha maisha yangu zaidi yakupona ukimwi, kwakweli hapana huyu sijui ni nani. Anataka nini,,aaah siku mjali niliendelea na mipango yangu,
Fuatilia bila kukosa jeee nani alepiga simu na je habiba atafanikiwa kutoroka
Habiba atakubali wito
Fuatiliaaa hapa hapa
Comments
Post a Comment