Sehemu ya 4
Ilipoishia toleo lililopita, " Habiba anachanganyikiwa baada yakupoteza dira ya maisha, kwa skendo na ugonjwa wa ukimwi anaoamini kua kevi ndio kamuambkiza, anapanga kutoroka kwao, ili aende kusiko julikana kwa jili ya kukwepa aibu na lawama, wakati yupo kwenye harakati hizo za kutaka kutoroka ghafla anapokea simu, na anapewa masharti kuwa wakutane magomeni saa tano asubuhi, na asijaribu kutokufika kwani atakuja kujutia, habiba haelewi ni nani anaongea nae wala kwanini kapewa ujumbe ule, anakua njia panda na haelewi la kufanya, anajikaza kwa kufanya maamuzi ya kuendelea kutaka kutoroka. Songa. Nayooo....." Aaah. Da kwani nimekosa nini mimi?,sijui nimekosea wapi maskini mbona mungu ananiadhibu, namna hii sina tabia ya umalaya lakini sasa naonekana malaya tena mwenye ukimwi tena nayetokea magazetini, ama kweli hujafa hujaumbika".....nilijisemea moyoni kwa uchungu sana, nilikua nimeanza kupaki mizigo yangu lakini niliacha kidogo nikaanza kuitafakari ile simu, sijui atakua mshenzi gani huyu aliepiga simu alafu eti anadai nikutane nae magomeni nisipoenda nitajutia, huyu jamaa fala kweli sijui vipi kwanza simjui alafuuuu" ......" nilisita kidogo nikajisemea kwa sauti ya chini chini ya kujutia kidogo"......."mamaaaaaaaaa. Mungu wangu sio kevi huyu ndio amepiga simu, daa sijui itakuaje anataka nini tena kwangu au kuna ishu imetokea tena?, ngoja, lakini mbona sio sauti yake kabisa,, .ngoja nimuulize James pengine atakua anajua yule mbwa anakaa wapi, maana huku mwananyamala simuoni sikuizi nahisi kahama, ,lakini james atakua anajua yupo wapi au anakaa wapi ngoja ni mdadisi kidogo"......"nilijikuta naongea mwenyewe nikiwa najiuliza nakujijibu mweywe ukiwa kwenye hali kama yangu, ngoja nikwambie, hupati, usingizi, huogi ukatakata, hupati hamu ya kula, kila mtu kwako ni adui, nakikubwa uoga na kuwaza kifo kila mara bila kusahau,hamu ya mapenzi inakua imekufa yaani kama mwanaume upo kwenye hali kama yangu, hata iyo mashine yako kusimama tena sahauu, nyie acheni tuu, sikia tu kua mtu anaukimwi ,, basi niliinyanyua simu yangu nikampigia james, ilikua usiku mida ya saa tatu ivi, james aliipokea simu yangu,, kiukweli jamani james simkubali kabisa yaani basi tu sijui nilikua nawaza nini, lakini sikutaka iwe topic kwasababu ndo nishaharibu tena basi mazungumzo yakawa hivi",,,,Habiba..."mambooo"......james "..poa tu mpenzi mambooo".....habiba ......"nimekumiss ile mbaya uko wapi baby"....james......." nipokitandani nakuwaza wewe"......"aaah yaani james alikua anajaribu kuleta hisia kwangu yaani angejua mwenzake waala hata sijali, mi nia yangu tuu, nikutaka kujua yule mpumbavu kevi anakaa wapi nipate uhakika kama ni magomeni au lah," habiba....." kweli mpenzi, unaniwaza mimi".?.....james...." haswaaa baby wangu wa dhati"....." wanaume waongo nyie sikutaka kujaji saaana nikaingia kwenye dhumuni"........."eti baby yuleeee, yuleee, naniiii, kevi. Nimemuona mitaa yetu tena, hivi anakaa wapi au ndio anausambaza ukimwi wake na huku kwetu"...."niliuliza swali kwa kujifanya namchukia kevi,nikweli namchukia lakini nilizuga chuki nilizipeleka kwenye kudadisi zaidi"..........james...." yaaaaa, yule jamaa kweli anaitwa kevi anakaa mwananyamala kwa mama zakalia, sasa ivi,, vipi umemjuaje jina baby"?......" james alinipiga swali ambalo sikutegemea nilichekecha kichwa upesiii nikajibu ,mwanamke , uongo hua haupotei kwangu,"....habiba....." anhaaaa nimeliona lile gazeti la ijumaa bwana si ndio kusoma ndani nikaiona picha yake na jina, kwaio ndio nikamjua jina gazetini".." mwanamke nikamaliza zoezi na swali gumu kwa jibu jepesi sana" ........james....." sawasawa. Basi ndio ivyo bwana yule jamaa apana chezea weka mbali na watoto ni silent killer kesha ua kibao nawengine anawatesa vitandani"....."daa yaani yale maneno yake james yalinikata maini sikua nahamu tena yakuongea nae, nilimjibu kua simu yangu haina chaji bettry low inakata sasa ivi,kwaio nilimuahidi nitampigia ikijaa chaji"......" shenzi kabisa utasubiri mpaka ukome sipigi tena simu" ..."nilisema kwa hasira sana,nikiwa chumbani kwangu" ...." hapo sasa nikawa nina mtihani tena sasa yule alie nipigia simu ni nani kama sio kevi?, aah nikaamua kuvunja ukimya nikamtumia meseji,, niliogopa kumpigia sauti yake unatisha alafu yupo serious sana, nikamtumia sms" ....." vipi we nani mwenzangu sikupati vizuri, sina namba yako alafu umesema tukutane magomeni kuna nini,?, nikaituma punde tu baada ya kumaliza, hazikupita dakika akatuma na yeye sms yake ilikua kama ifuatavyo," ....." wewe ukifika magomeni saa tano utapata majibu yote hayo"......"duu huyu mtu ni jambazi au? mbona hivi tena, basi sikutaka kujifanya najua sana maana nilijifanya najua kupenda nikaumbuka,, ngoja tu kesho ifike nikakutane naye huyu mpuuzi sijui kuna nini" ....." usingizi unakuja basiiiii!! mbwembwe tuu yaani full kuesabu nondo, daa we acha tuu",......kesho yake mungu akajaalia ikafika sina tena u sister duu nilikua nimeshapagawa yaani basi tu no saloon. No kula kula, yaani mungu huyu kwakweli yeye pekee ndio anajua navyoteseka, nilijiandaa haraka haraka, nikawa napita sitting room, ghafla baba akaniita, nilitukana kimoyo moyo, siwez sema ni tusi gani,," "daa huyu naye anataka nini sijui"..."nilijikuta na mzalau baba yangu mzazi ila sikujali mimi ndio nilikua mtu mwenye matatizo makubwa kuliko yeye anayelisha familia kwaio sikujali kabisaa."..
......baba....."habiba vipi wapi tena".?..
..."aliuliza ikabidi nijibu tuu kwa kuongopa ndio maisha yangu hayo ya kila siku ukweli nausema moyoni mdomoni uongo tupu"...
."natoka naenda kwa rafiki yangu"....."nilijibu kwa ufupi tuu".....
...baba.....".mbona mapema sanaaa?" ....
" daa yaani angejua ananichelewesha kuwahi magomeni na kifoleni hiki cha asubuhi asinge thubutu kunigasi".
....habiba...."kuna kazi naenda kumsaidia rafiki yangu"....
..baba....." sasa mwanangu kunasehemu nataka twende sio mbali sana ila naahidi kukuwahisha kwa huyo rafiki yako sitokuchelewesha," .
..." .daa huyu mzee hajui alitendalo, nilimalizia neno langu la moyoni nilimkubalia kwa kichwa"......" kumbe alikua kesha waambia na wakina batuli kuwa leo tunatoka nikamuona mamkubwa na Batuli nao wamevaa safi wanakuja tulipo mimi n! Baba,"...
...baba...." haya twendeni tuwahi jamani".....
." sijui tunaenda api au shamba maana asije akafanya nichelewe huyu kwa yule jamaa Wa magomeni" nilijisemea moyoni kama kawaida yangu"....
...baba......"haya tumefika jamani" ......"baba alituambia tushuke kwenye gari tumfuate sikujua ni wapi tunaelekea lakini nikama kwenye hospitali iv ila sikujali wala nini, nilijua kutakua kuna mgonjwa amekuja kumuangalia,, mara tukakaa kwenye benchi lile la wagonjwa sikumuelewa baba ni nini kimetuleta na hamna alieuliza kitu kila mtu alikua anangoja kuona nini kinaendelea ghafla alikuja nesi akamchukua baba na kwenda nae mpaka chumba flani sikujali pia,, baada ya muda kama dakika kumi na tano mzee alitoka akiwa ameshikilia kapamba kadogo mkononi juu kidogo ya paja la mkono, nikama alikua kaenda kutoa damu hivi,ghafla alikuja tena yule nessi, akaja kumchukua Batuli, nae vile vile akaja kama baba na pamba yake akiwa anaskia viuchungu kidogo vya kutobolewa,wakati nashangaa yote hayo ikabidi nimuulize mzee" ......"baba vipi mnaumwa au mbona mmeenda we na batuli kutoa damu"..." mzee kabla hajajibu alikuja tena yule nessi kisha akaniamuru nimfuate nikamuangalia baba ,baba nae akanipa ishara kua niende naye basi nikamfuata, kufika kule nikakutana na dokta akaanza kupiga stori na mimi sikuelewa kamchezo kanaendaje ghafla nikaanza kuambiwa, sijui nisihofu nivizuri nimekuja kuangalia afya yangu na kwamba. Vipimo vitakua siri kati yangu na yeye,"
"mungu wangu leo nimekamatwa mkojo ukaanza kubana haja pia ikaanza kubana,yaani kumbe mbwembwe zote zile kumbe ni kupima ukimwiiiiii, leo naumbuka mimi, habiba yamenikuta"
...."nyie acheni tuu nilianza kulia pale pale tena kwa nguvu,, dokta akanibembeleza kisha wakaanza kunihoji maswali yao, niliongopa kila kitu kisha nikaomba ruksa yakwenda chooni walikua wamesha aanza kunitoa damu yule dokta baada yakumaliza , aliniruhusu niende cbooni kisha nirudi kuchukua majibu yangu,",
" nani wakurudi labda sio mimi na hii ndio tiketi yakuondokea nakutoroka sina tena mpango wakubaki"....kimoyo moyo nilitamka huku nikiwa natoka mule ndani kwa dokta, nilitafuta mlango wapili wakutokea kisha nikaanza kuondoka zangu kuelekea nyumbani waache wasubiri ila mimi sipo tena dar es salaam hii, nilirudi kuchukua begi langu languo kisha nikaanza safari yakwenda kwanza magomeni, nyumbani alikua kabaki mfanyakazi tuuu ,alikua yupo na mtoto,, sikumjali na hakuuliza kwanini nimerudi peke yangu, nilichukua kila kilicho changu nachoweza kubeba nikatimua mbio, pesa nilikua nayo ya nauli na matumizi ilikua kama laki mbili na nusu hivi ,baba alinipa nikanunue simu lakini sikununua nilikua nina mipango nayo mingine kabisaaa, nikachukua gari za kariakoo kwakua nilitokea nyumbani, basi mojakwa moja ikaanza safari ya magomeni, bahati nzuri foleni ilikua sio kubwa sana hivyo nikawai kufika pale magomeni, niliposhuka tuu nikampigia jamaa simu kumuuliza yupo wapi?"
" vipi. Mimi nimesha fika wewe upo wapi naumevaaje" ...."nilimuuliza nipate uhakika" .........
....." nipo mbele yako nimevaa t. Shirt jeusi" ......."jamaa lilijibu upesi nikashtuka kugeuka tu nikakutana nae"....
Itaendelea leo hiiii
Fuatia jamaa ni nani. Na anataka nini
Vipi vipimo alivyopima na kukimbia majibu
Comments
Post a Comment