Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola huenda akatambua kocha mpya ajae wa timu ya Bayern Munich inayoshiriki ligi kuu ya Bundesliga.
Bayern Munich ilimfungashia virago kocha wake Carlo Ancelotti wiki iliyopita kufuatia kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Paris Saint-Germain michuano ya klabu bingwa barani Ulaya huku ikitoka sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Hertha Berlin mwishoni mwa wiki.
Guardiola, ambaye amekuwepo Allianz Arena kwa miaka mitatu ya mafanikio kabla ya kuondoka na kuamia Manchester City mwaka uliyopita Jumanne hii amekutana na rais wa Bayern, Uli Hoeness jijini Munich.
Rais huyo wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesema kuwa tayari ameshamuambia Pep Guardiola siku ya Jumanne walipokutana katika mgahawa huko Munich ni kocha wa ainagani atapata nafasi ya kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti.
Hoeness ameliambia gazeti la Abendzeitung kwamba maamuzi yamependekezwa na Ancelotti na Guardiola amethibitisha hilo.
Uli Hoeness amesema kuwa “Huwa tunakutana kila mwezi Oktoba kubadilishana mawazo kama marafiki na nimemuambia ninani tunatarajia kumteua kuwa kocha mpya siku chache zijazo na ameridhia.”
Mpaka sasa makocha ambao wanapigiwa upatu kupata nafasi hiyo ni Thomas Tuchel, Louis van Gaal, Luis Enrique na Julian Nagelsmann.
Comments
Post a Comment