Msanii wa muziki Bongo, Aslay ameeleza sababu ya kutoa nyimbo mfululizo.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Natamba’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa anataka kuwa na nyimbo nyingi ila anapokuwa anafanya show zake asitumie nyimbo za Yamoto Band.
“Tangu nimetoka kwenye band nimekuwa nikifanya kazi peke yangu natengemea show zangu ziwe na nyimbo zangu tu siyo za Band ndio maana nafanya kutoa nyimbo nyingi ilimradi hata nikipata show niwe natumia nyimbo zangu,” amesema Aslay.
“Kingine natoa kazi nyingi kwa sababu ni nzuri, kazi nzuri ikikaa ndani huwa naogopa kwa sababu naogopa idea kugongana, kazi nuri ukitoa leo nyingine ukatoa kesho watu watapenda tu” ameongeza.
Kwa mwaka huu Aslay amefanya vizuri na ngoma kama Mhudumu, Baby, Angekuona, Tete, Pusha, Marioo, Likizo, Danga na nyinginezo.
Comments
Post a Comment