Klabu ya soka ya Leicester City ya nchini Uingereza, imekataliwa ombi lake la kuhitaji mchezaji, Adrien Silva kujiunga na timu hiyo baada ya kumsajili nje ya muda kwa dau la paundi milioni 22 akitokea Sporting Lisbon.
Shirikisho la mpira wa miguu duniani ‘Fifa’ limeikatalia timu hiyo ya Leicester ambayo iliwasilisha stakabadhi FA za kumsajali mchezaji huyo wakiwa wamechelewa kwa sekunde 14 wakati wa siku ya kukamilika dirisha la usajili Agosti 31.
Kutokana na timu hiyo kukataliwa sasa Leicester wataweza kumjumuisha Silva kikosini msimu ujao wa usajili mwezi Januari.
Leicester City ipo nafasi ya17 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa imeshinda mchezo mmoja pekee mpaka sasa.
Comments
Post a Comment