Mbinu za Kukabiliana na Ugumu wa Maisha


Mbinu za kuyakabili maisha hazijabadilika tangu zama hizo hela ianze kushika mkondo: tafuta pesa, bana matumizi, hifadhi ziada, na wekeza kwa umakini.
Ili kufanikisha hayo, fanya yafuatayo:-
1. Acha matumizi/manunuzi yasiyo ya lazima, mf. kunywa soda/bia nyingi kwa siku, kutoa ofa zisizo
na msingi, kununua chai kwenye mighahawa wakati unaweza kupata ofisini/au nyumbani, kula ovyo barabarani (pipi, karanga, ..) hata
kama huna njaa.
2. Fanya tahmini juu ya bei nafuu na upatikanaji wa bidhaa bora. Andaa orodha ya vitu unavyotaka kununua kabla hujaenda sokoni/dukani/ na kujikita katika orodha yako tuu.
Usinunue usichopanga. Pia tunza kumbukumbu za manunuzi ya wiki, mwezi,.. na ipitie orodha yako kabla ya kufanya manunuzi/kuanza wakati unaofuata. Hii itakuwezesha kufanya tahmini wakati wa kutaka kuondoa baadhi ya vitu, kwakuwa havikuwa vya lazima.
3. Punguza matumizi ya umeme/maji. Mf. kutokuacha redio/tv inawaka siku nzima, laptop kwenye charge wakati hautumii, kutengeneza bomba za maji zinazovuja, kuoga kwa kutumia shower, sambamba na kuoga haraka si lazima utumia dk 30 bafuni.
4. Punguza matumizi ya simu kwa kutokupiga simu zisizo na ulazima. Unaweza kujiunga na vifurushi vya gharama nafuu kwa siku/wiki hata
mwezi. Ikiwa kama hakuna ulazima usijiunge.
5. Punguza safari zisizo na tija, Kwa wenye magari, unaweza kutumia usafiri wa daladala kwenda sehemu panapofikika kwa urahisi. Pia, tembea kwa miguu (TZ11) ukiwa mtaani, punguza gharama za mafuta kwa kuendesha taratibu.

6. Punguza starehe zinazogharimu. Mf. kwenda movie kila siku, bia sehemu za kifahari (bia 1 – 4,000), kuhudhuria tafrija/sherehe zisizokulazimu.
7. Nunua vyakula (unga, sukari, ..) kwa bei ya jumla sokoni na kuhifadhi nyumbani hususani visivyoharibika, kwa vinavyoaharibika, nunua kiasi visije kuharibika, pika pika kiasi
kinachotosha wakati husika, na kikibaki hifadhi (usitupe chakula wala usisaze), unaweza kwenda
ofisini na lunch box,
8. Nunua sabuni za jumla dukani, natumia kwa uangalifu. Kiasi kidogo cha sabuni za kufulia na kuogea kinatosha. Nunua bidhaa (manukato,
nguo, viatu,..) utakazokua unatumia tuu, mf. kuna watu wana aina 6 za perfume tena za gharama. Kununua vitu na kukihifadhi haina maana na ni upotezaji wa pesa.
9. Jiunge kwenye bima mbalimbali. Mf. Bima za afya, maisha, nyumba, gari, zenye manufaa kwako, na fanya uchunguzi kabla ya yote, bila kusahau mifuko ya akiba (pensheni).
10. Nunua vitu vilivyotumika (second hand), kwa namna fulani vinapunguzo la gharama. Mf.
gari, tv, baiskel, laptop. Hakikisha vipo katika hali nzuri inayoridhisha, ikiwa vinayo waranti ni bora zaidi.
11. Lipa bili zako kwa wakati, bila kusahau madeni uliyokopa kwa watu. Ukiona unazidishiwa gharama kwenye bili zako uliza. Epuka kulipia kitu ambacho hujatumia kwa uhalali. Bila kusahau kuacha chenji kwa
barmaid, iwe mwisho.
12. Epuka kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kwa mfano, kununua muda wa maongezi kutoka benki, credit card, kulipia huduma kwa kadi za benki. Lipa kwa fedha
taslimu uone thamani na maumivu ya kutoa pesa.
13. Unapoona fursa yoyote itakayokupunguzia gharama itumie ipasavyo. Mf. punguzo la bei, mnada, Usisite kuomba punguzo la bei hata kama ni supermarket na fixed bei zao, kuwa mbishi.
14. Acha kabisa matumizi ya vitu/vilevi vya gharama vitakavyokufanya kuwa mtumwa. Mf. madawa ya kulevya, pombe, sigara.
15. Fungua akaunti mbili benki, akaunti ya matumizi na kaunti ya kukusanyia mtaji wa uwekezaji. Ili kupunguza gharama, kaunti zote
zisiwe gharama za uendeshaji i.e makato ya mwezi (hususani akaunti ya kukusanyia fedha za uwekezaji). Hakikisha kila mara unaweka kiasi
cha fedha kwenye akaunti hizo. Katika kila mapato yako, weka siyo chini ya 20% katika akaunti ya uwekezaji. Pia weka chenji za sarafu katika kibubu.
16. Wekeza pesa uliyokusanya katika mradi wowote ili kujiongezea kipato. Fanya tathmini (andisha mpango wa biashara yako i.e Business Plan). Usifanye biashara kichwa kichwa, au kuiga kutoka kwa marafiki. Pia unaweza kuuza vitu
vidogo vidogo sehemu unayoishi/kufanyia kazi. Mfano, kuuza maji ya baridi, chapati, maandazi, karanga, ice cream/barafu, … Hapa utaepuka kodi, pia vinakuongezea marafiki.
17. Saidia wahitaji. Kujigharamia peke si sehemu ya maadaili katika jamii yoyote ile! Jitahidi kutoa msaada kwa watu wanohitaji kwa dhati msaada kutoka kwako. Mfano, kuwasaidia yatima, wagonjwa wasio na msaada, kutembelea wazee. Kufanya hivyo kutafupa faraja ya kweli, na watakuombea upate baraka zaidi. Jitahidi usiwape msaada watu wanaokwepa kujituma/kutofanya kazi. Hii
inawadumaza, na kuwafanya kuwa tegemezi wa kudumu.
18. Ishi kilimo kwanza. Unaweza kuotesha miche kadhaa ya nyanya miongoni mwa maua yako ya nyumbani, kuotesha miti ya matunda itakayokupatia kivuli na matunda, minazi. Usikubali kuotesha mimea yenye faida moja tu, mf. mapambo au kivuli, nyumbani kwako.

Comments