Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri anayecheza club ya Liverpool ya England Mohamed Salah jina lake limezidi kuchukua headlines kiasi cha kudaiwa kutaka kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Misri.
Mohamed Salah anadaiwa kutaka kufanya hivyo baada ya picha yake kiongozi wa kisisa wa Chechen Mr Ramzan Kadyrov kusambaa mitandaoni na kuanza kumkosoa staa huyo kwa kudai anatumika kisiasa, Ramzan ni kiongozi wa jimbo la Chechen nchini Urusi na amekuwa akidaiwa kuwa na sifa ambazo sio nzuri.
MO Salah akiwa na Ramzan |
Mashabiki wa soka nchini Misri baada ya kusikia taarifa za MO Salah kutaka kuachana na timu ya taifa kwa kuandamwa na maneno baada ya picha yake na Ramzan kusambaa, wameanza kupost ujumbe wenye #IamWithSalah kama njia ya kuonesha wapo pamoja nae na wasingependa astaafu, kama ufahamu timu ya taifa ya Misri imekuwa Chechen nchni Urusi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia.
Comments
Post a Comment